Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rubani wa helkopta iliyotua kimakosa Darfur amepatikana leo akiwa salama

Rubani wa helkopta iliyotua kimakosa Darfur amepatikana leo akiwa salama

Rubani wa helkopya inayomilikiwa na Urusi aliyetua kimakosa Darfur Sudan leo amepatikana akiwa salama salimini.

Kwa mujibu wa mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika Darfur UNAMID Rubani huyo, abiria saba na wafanyakazi wa ndege walitua kimakosa Darfur mwanzoni mwa wiki. Wengine wote walipatikana salama na kusafirishwa hadi mjini Elfasher isipokuwa rubani. Mkuu wa UNAMID Ibrahim Gambari amesema  hatimaye jioni hii wamefanikiwa kumpata akiwa salama na kumpeleka Nyala .

Helkopta hiyo ilitoweka siku ya Jumatatu ilipokuwa ikiwasafirisha wajumbe watatu wa kundi la waasi la Liberation Justice Movement LJM kutoka kwenye mazungumzo ya amani na serikali ya Sudan mjini Doha Qatar. Wajumbe hao walikuwa wanaelekea Sudan Kusini lakini wakajikuta wametua Darfur, na walichukuliwa na helkopta nyingine hadi hadi El-Fasher.