Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa baraza la usalama ahuzunishwa na ajali ya boti DR Congo

Rais wa baraza la usalama ahuzunishwa na ajali ya boti DR Congo

Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Ali Treki leo ameelezea huzuni yake kufuatia ajali ya boti kwenye mto Congo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuuwa watu takribani 140.

Duru za habari zinasema boti hiyo ilizama jana ikisafirisha abiria na mizigo kwenye kando ya mto Kasai ambao ni tawi la mto Congo kutoka eneo la Mushie kwenda mji mkuu Kinshasa. Inasemekana boti hiyo ilijaza watu na mizigo kupita kiasi.

Wakongo wengi wanasafiri kwa boti hata kama ikiwa imejaa kupita kiasi kutokana na uhaba wa reli na barabara zinazofanya kazi. Katika taarifa yake Rais wa baraza Ali Treki amezielezea habari hizo za kuzama kwa boti kama ni za kushtua na ametoa salamu za rambirambi kwa familia za waliokufa, watu wa Congo na serikali.