Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kulipa dola milioni 650 kama fidia kwa waathirika wa uvamizi wa Iraq Kuwait

UM kulipa dola milioni 650 kama fidia kwa waathirika wa uvamizi wa Iraq Kuwait

Tume ya Umoja wa Mataifa ya fidia UNCC ambayo hushughulika na kulipa madai ya walioathirika kutokana na uvamizi wa Iraq Kuwait 1990 leo imetoa dola milioni 650 kama fidia kwa madai tisa.

Baraza la UNCC limegawanda madai hayo katika ngazi sita, manne ni ya watu binafsi, moja ni la mashirika la moja ni la serikali na mashirika ya kimataifa ambayo pia yanahusisha madai ya uharibifu wa mazingira.

Kwa mujibu wa UNCC malipo hayo ya leo yanafanya jumla ya fedha za fidia zilizotolewa na tume hiyo kufikia zaidi ya dola bilioni 30. Tangu ilipoanzishwa mwaka 1991 tume hiyo imeshapokea madai karibu milioni tatu yakiwemo takribani 100 kutoka kwa serikali, raia wao au mashirika.