Skip to main content

Watoto wa Gaza wajaribu kuvunja rekodi nyingine ya dunia kurusha tiara

Watoto wa Gaza wajaribu kuvunja rekodi nyingine ya dunia kurusha tiara

Watoto wa Gaza wanaoshiriki michezo ya kiangazi inayofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA wanajaribu kuvunja rekodi nyingine ya dunia .

Watoto hao ambao wiki iliyopita walivunja rekodi ya dunia ya kudundadunda mpira wa kikabu ,leo kwa maelfu wanajaribu kuvunja rekodi yao ya dunia ya kurusha tiara au kishada kwa pamoja.

Zaidi ya watoto 3000 ambao wanashiriki michezo ya UNRWA walivunja rekodi ya dunia iliyokuwepo ya kurusha kishada mwaka mmoja uliopita. Chrispopher Gunnes ni msemaji wa UNRWA hamsa ya watoto hao kuvunja rekodi.

(SAUTI YA GUNNES)