Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makaburi ya ufalme wa Baganda ni urithi wa dunia ulio hatarini:UNESCO

Makaburi ya ufalme wa Baganda ni urithi wa dunia ulio hatarini:UNESCO

Makaburi ya wafalme wa Baganda yaliyopo Kasubi nchini Uganda yameorodheshwa miongoni mwa urithi wa dunia ulioko hatarini.

Makaburi hayo yamejumuishwa katika orodha hiyo na mkutano wa 34 wa kamati ya urithi wa dunia ulioongozwa na waziri wa utamaduni wa Brazil Joao Luiz da Silva Ferreira. Pia kamati hiyo imeamua kuvitoa visiwa vya Galapagos vilivyoko Ecuador kutoka kwenye orodha hiyo. Machi mwaka huu moto mkubwa karibu uteketeze kabisa jingo la Muzibu Azaala Mpanga ambalo ndio kubwa na wafalme wane wa Baganda wamezikwa humo.

Makaburi hayo ambayo ni mfano mzuri wa ubunifu wa kihandisi wa ufalme wa Baganda yalijengwa karne ya 13 na sasa yatakarabatiwa upya. Navyo visiwa vya Galapagos ambavyo vimekuwa vikielezwa kama makumbusho ya aina yake viliwekwa kwenye orodha hiyo mwaka 2007 kwa sababu ya tishio lililotokana na kuingiliwa na viumbe vingine, utalii na uvuvi. Lakini sasa kamati inasema hatua kubwa zimepigwa na serikali ya Ecuador kutatua matatizo hayo na ndio maana imeondolewa kwenye orodha ya urithi ulio hatarini.