Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miradi ya UM ya kulinda misitu yasaidia kupunguza uharibifu Tanzania

Miradi ya UM ya kulinda misitu yasaidia kupunguza uharibifu Tanzania

Maelfu ya ekari ya misitu kaskazini mashariki ya Tanzaina imehifadhiwa kutokana na mradi wa wa miaka saba uliokamilika hivu maajuzi wa kulinda misitu uliotekelezwa na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP.

Mradi huo uliofadhiliwa na idara inayohusika na mazingira duniani GEF ulikamilika mwezi uliopia baada ya uchunguzi huru kueleza kuwa takriban ukari 10,000 za misitu zimeokolewa kutokana na uharibifu huku asilimia ya kupotea kwa misitu ikipungua kwa asilimia kumi .

Serikali ya Tanziania ilipendekeza msitu huo kutambuliwa na shirika la umoja wa mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO kama eneo la kitamaduni. Shirika la UNPD lilitekeleza miradi huo kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania , mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na wasimamishi wa vijiji kama njia ya kuijumuisha jamii katika utunzaji wa misitu.