Skip to main content

WFP yaahidi kulisaidia bara la Afrika katika kujitegemea kwa chakula

WFP yaahidi kulisaidia bara la Afrika katika kujitegemea kwa chakula

Umoja wa mataifa umetangaza kuwa una mpango wa kuyasaiadia mataifa ya afrika kukabiliana na njaa na utapia mlo na pia kuliwezesha bara la afrika kuwa na chakula cha kutosha.

Akiwahutubia marais wa mataifa ya bara la afrika kwenye mkutano wa muungano wa Afrika AU uliondaliwa kwenye mji mkuu wa Uganda Kampala, mkurugenzi mkuu wa shirika la mpamgo wa chakula duniani WFP josette Sheeran amesema kuwa kuna manufaa mengi yanayotaka na mipango ya matumizi chakula miongoni mwa jamii itasaidi kukabiliana na njaa na pia kuchangia kumarika kwa kilimo na kukua kwa uchumi kwa haraka.

 Josette pia amesema kuwa mpango huo utasaidia vyakula kufika sokoni hasa kuwafikia wanaovihitaji na pia kusaidia kuimarika kwa miundo mbinu kama vile barabara. Amesema kuwa mpango huo ambao unatekelezwa katika nchi kumi na sita za bara la afrika utayainua maisha ya jamii za vijini kote barani.