mafuriko yakatili maisha ya watu wawili na kuharibu makazi kusini mwa Sudan

mafuriko yakatili maisha ya watu wawili na kuharibu makazi kusini mwa Sudan

Takriban watu wawili wameuawa na zaidi ya makaazi 130 kuharibiwa kwa muda wa siku kumi zilizopita kutokana na mafuriko yanayobabishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika jimbo la Jonglei kusini mwa sudan.

Kulingana na ripoti ya Shirika la mpango wa chakula dunia WFP ni kuwa wale walioathirika na mafuriko hayo kwa sasa wanakabiliwa na ukosefu wa makao , chakula pamoja na maji safi ya kunywa. Inakisiwa kuwa mafuriko hayo yataendelea kushuhudiwa hadi mapema mwezi septemba kulinga na kiwango cha mvua kitakacho shuhudiwa wakati huo .

Ripoti hiyo ya WFP pia inasema kuwa makundi ya kutoa huduma za kibinadamu yatakuwa yakichunguza hali ikiwa kutakuwa na dalili zozote na mkurupuko wa maradhi.