UM waipongeza Namibia ilivyokabiliana na homa ya bonde la ufa

UM waipongeza Namibia ilivyokabiliana na homa ya bonde la ufa

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa ameipongeza serikali ya Namibia kwa hatua ilizochukua kuzuia kusambaa kwa homa ya bonde la ufa iliyozuka hivi karibuni, na kusema nchi nyingine zinaweza kujifunza kutokana na uzoefu wa Namibia.

Afisa huyo mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilomo FAO Jacques Diouf akizungumza katika mkutano mjini Windhoek nchini humo amesema huu ni mfano wa kuigwa na nchi zingine ili kuwalinda wanyama, maisha, biashara na watu, pia nchi jirani kutokana na ugonjwa huu. Homa ya bonde la ufa ilizuka Namibia mwezi Mai baada ya kutokuwepo kwa miaka 25.

 Ugonjwa huo unabebwa na mbu baada ya kunyesha mvua kubwa na mafuriko na dalili zake ni kutoka kwa mamba nyingi na kuzaa kabla ya wakati wa wanyama kama kondoo, mbuzi na ng'ombe. Binadamu pia wako katika hatari na wanaweza kufa na ugonjwa huu, hasa wakigusana na damu au viungo vya wanyama walioambukizwa, au kuumwa na mbu aliyebeba ugonjwa huo.