Rubani wa helkopta iliyotua kimakosa Darfur bado hajapatikana

Rubani wa helkopta iliyotua kimakosa Darfur bado hajapatikana

Rubani wa helkopya iliyomilikiwa na Urusi aliyetua kimakosa Darfur Sudan bado hajulikani aliko mpaka sasa.

Abiria saba waliokuwa ndani ya helkopta hiyo na wafanyakazi wa ndege wamepatikana wakiwa salama na kusafirishwa hadi mjini Elfasher. Helkopta hiyo ilitoweka siku ya Jumatatu ilipokuwa ikiwasafirisha wajumbe watatu wa kundi la waasi la Liberation Justice Movement LJM kutoka kwenye mazungumzo ya amani na serikali ya Sudan mjini Doha Qatar.

Wajumbe hao walikuwa wanaelekea Sudan Kusini lakini wakajikuta wametua Darfur. Ndege nyingine ilitumwa kwenye eneo hilo na kuwachukua abiria, wafanyakazi na helkopta hiyo hkuwapeleka hadi El-Fasher. Mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa na wa Afrika Darfur UNAMID Ibrahim Gambari amesema juhudi zinaendelea kufanyika kumtafuta rubani huyo.