Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imefikisha msaada kwa waathirika wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

UNHCR imefikisha msaada kwa waathirika wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Wafanyakazi wa misaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wamefanikiwa kuyafikia maeneo ya vijijini ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo ilikuwa vigumu kuyafikia .

Maeneo hayo imeelezwa kuwa yameghubikwa na matatizo ya utapia mlo kwa watoto, vitendo vya ubakaji na ghasia. Kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR Fatouma Lejeune-Kaba sasa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imeidhinisha wafanyakazi hao kuingia eneo la Ndebele lililoko kilometa 600 Kaskazini mwa mji mkuu Bangui baada ya kuzuiliwa kuingia huko tangu Desemba kwa sababu za kiusalama.

(SAUTI YA  FATOUMA -CAR)

Fatouma anasema UNHCR na washirika wake hivi sasa wanatathimini mahitaji ya watu na usalama katika eneo hilo na kuruhisiwa kwao ni muhimu sana.