Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi wa UNDP yuko ziaran Brazili kuchagiza malengo ya milenia

Mkurugenzi wa UNDP yuko ziaran Brazili kuchagiza malengo ya milenia

Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP Helen Clark leo ameanza ziara ya siku mbili nchini Brazil.

Katika ziara hiyo anatarajiwa kutia sahihi mkataba wa miapango ya ushirikiano baina ya shirika lake na serikali ya Brazil, ikiwa ni pamoja na masuala yanayoambatana na juhudi za kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

Kabla ya kuhitimisha ziara yake Bi Clark atakuwa na mkutano na Rais Luiz Inacio Lula da Silva, balozi Celso Amorim, waziri wa mambo ya nje wan chi hiyo Bi Isabella Teixeira, waziri wa mazingira na maafisa wengine wa ngazi ya juu katika serikali ya Brazil.