Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maridhiano na diplomasia ni suluhu kubwa ya mizozo duniani:UM

Maridhiano na diplomasia ni suluhu kubwa ya mizozo duniani:UM

Upatanishi wa amani na diplomasia vimetajwa kuwa njia kubwa za kusuluhisha mizozo duniani.

Haya yamesemwa na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kisiasa Lyn Pascoe ambaye pia amesema kuwa Umoja huo utaanza kutumia njia za kidiplomasia kutuliza hali kabla ya mizozo kutokea.

Pascoe Amesema umoja huo una mipango ya kuzuia kuanza kwa ghasia na kuongeza kuwa upatanishi unahitajika kumaliza vita na kusaidia mataifa au pande zinazozozana kuafikiana hasa wanaokabiliwa na hali ngumu ya kisiasa.

Pascoe ametoa mfano wa ghasia zilizotokea nchini Kenya mwaka 2007 na mwanzoni mwa 2008 baada ya uchaguzi mkuu kama moja ya upatanishi na njia ya kidiplomasia ilivyotumika kupitia kwa Umoja wa Mataifa kutuliza hali hiyo.