Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto milioni nane kupewa chanjo ya ya kuzuia polio nchini Afghanistan

Watoto milioni nane kupewa chanjo ya ya kuzuia polio nchini Afghanistan

Zaidi ya wahudumu wa afua 20,000 wa kujitolea wanaendelea kuzuru nyumba hadi nyumba wakitoa chanjo kwa watoto dhidi ya polio nchini Afghanistan kama moja ya kampeni ya Umoja wa Mataifa ya kuwachanja watoto milioni 8 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Afisa mkuu wa shirika la afya duniani WHO katika mkoa wa Kandahar kusini , Rahmathula Kamwark amesema wanatarajia kuwa huenda wakapata msaada kutoka kwa wasomi wa dini, wawakilishi wa jamii, wazazi pamoja na watu wa kawaida ili kutimiza lengo lao la kuangamiza ugonjwa wa polio katika eneo hilo.

Kamwark ameyasema hayo jana wakati wa sherehe za ufunguzi wa kampeni hiyo ya siku tatu ambayo inawatuma watu 20,000 kuzuru nyumba hadi nyumba kutoa chanjo kwa watoto walio chini ya miaka mitano kwenye mikoa 14 kati ya miko 34 nchini Afghanistan.