Skip to main content

Mchakato wa amani wa Darfur umefika katika hali ngumu na nyeti:UM

Mchakato wa amani wa Darfur umefika katika hali ngumu na nyeti:UM

Mwakilishi maalumu wa mpango wa kulinda amani Darfur wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID Ibrahim Gambari leo amelieleza baraza la usalama kuhusu hali ya jimbo hilo la Sudan.

Amesema hali ya usalama inazidi kuzorota ingawa wakati huohuio UNAMID inakamilisha mipango ya mazungumzo ya kisiasa ndani ya Darfur ili kuunga mkono juhudi za amani za Doha. Amesema mchakato wa amani umepata nguvu mpya kwa makubaliano ya karibuni ya amani baina ya serikali na kundi la Liberation and Justice Movement LJM.

Hata hivyo Bwana Gambari amesema kuna hofu kuhusu ongezeko la vitendo vya kihalifu na mashambulizi dhidi ya Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa misaada, japo kuna matumaini kuwa hali ya usalama na makubaliano ya amani yana ishara nzuri.

(SAUTI IBRAHIMU GAMBARI)