Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya misaada leo yametoa wito mpya wa msaada kwa ajili ya Kyrgystan

Mashirika ya misaada leo yametoa wito mpya wa msaada kwa ajili ya Kyrgystan

Wadau wa misaada nchini Kyrgyzstan leo wametoa wito mpya wa dola milioni 96 kwa ajili ya kuwasaidia eneo la kusini mwa nchi hiyo kulikozuka machafuko mwezi Juni na kuathiri watu 400,000.

Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Anthony Lake amesema hali ya kisiasa imetulia lakini maisha ya watoto bado yako mashakani. Amesema kuna hatari ya kusahau usalama wa watoto takriban 100,000 walioathirika na mchafuko.

Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa wito wa kuboresha hali na kuwezesha kurejea kwa wakimbizi wa ndani 75,000 na linahitaji dola milioni 23 kufanikisha hilo. Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA  MELISA-UNHCR)