Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia isiyo na silaha za nyuklia ni hakikisho la usalama kwa wote: Ban

Dunia isiyo na silaha za nyuklia ni hakikisho la usalama kwa wote: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametoa wito wa juhudi zaidi za kimataifa za ajenda ya kutokomeza silaha za nyukilia, akisisitiza kwamba kufanya hivyo ni njia pekee ya kuhakikisha usalama kwa wote.

Amesema tuwe bayana, kwamba hakikisho pekee la usalama na njia ya uhakika ya kujilinda dhidi ya matumizi ya silaha hizo ni kuzitokomeza. Ban ameyasema hayo leo katika ujumbe maalumu kwa mkutano ulioanza wa Hiroshima kwa ajili ya kutokomeza silaha za nyuklia ifikapo 2020. Hiroshima ni moja ya miji miwili ya Japan ambayo Marekani ilishambulia kwa bomu la nyuklia wakati wa vita ya pili ya dunia.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky amesema Katibu Mkuu amewataka viongozi wa dunia hususan wale ambao nchi zao zinamiliki nyuklia kuzuru Hiroshima na Nagasaki kujionea bayana athari za vita vya nyuklia.

(SAUTI YA NESIRKY )

Mkutano huo wa siku tatu umeandaliwa na mameya kwa ajili ya amani ambao unajumuisha mameya zaidi ya 4000 na maafisa wengine wa miji, ukiwa na lengo la kuwa na dunia isiyo na silaha za nyuklia.