Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF imezindua duru nyingine ya chanjo kwa watoto nchini Haiti

UNICEF imezindua duru nyingine ya chanjo kwa watoto nchini Haiti

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limezindua awamu nyingine ya chanjo kwa watoto nchini Haiti.

Kwa mujibu wa msemaji wa UNICEF watoto laki tano wanatarajiwa kupewa chanjo ya dharuda katika duru ya pili ya kampeni hiyo. Pia amesema mbali ya kupewa chanjo watu milioni 1.2 hivi sasa wameweza kufikiwa kupata maji safi na salama na maelfu ni watoto. Pia watoto 63,000 nchini Haiti hivi sasa wanapata msaada wa kisaikolojia ili kuwachagiza kurejea katika maisha ya kawaida.

Ameongeza kuwa hali ya lishe imeimarika sana na hakuna taarifa mpya za watoto kukumbwa na utapia mlo, jambo ambalo ni la kutia moyo ukilinganisha na athari na hali halisi ya baada ya tetemeko nchini Haiti.