Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa AU waafikiana kuongeza vikosi vya kulinda amani nchini Somalia

Viongozi wa AU waafikiana kuongeza vikosi vya kulinda amani nchini Somalia

Mkutano wa 15 wa viongozi wa nchi za umoja wa Afrika AU uliomalizika leo mjini Kampala Uganda umeafikiana kuongeza majeshi zaidi ya kulinda amani nchini Somalia.

Viongozi hao wameamua kupeleka wanajeshi 2000 zaidi katika mji mkuu wa Somalia Moghadishu. Pia viongozi hao wamesema sasa uwezo wa vikosi vyao Somalia utabadilika ili kuwawezesha kukabiliana na wanamgambo iwapo watashambuliwa.

Awali Rais Yoweri wa Uganda alitoa wito wa kuongeza vikosi kukabiliana na wanamgambo wa Al-Shabab, kundi lililokiri kufanya shambulio la kigaidi Uganda hivi karibuni. Umoja wa Mataifa umekuwa msitari wa mbele kushirikiana na AU kuhakikisha usalama wa raia unalindwa Somalia. Mwakilishi mpya wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ni Balozi Augustino Mahiga anafanua kuhusu hatua hiyo ya AU.

(SAUTI YA  MAHIGA )