Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwekeza kwa wanawake kuna faida kubwa kwa kizazi hiki na kijacho:Migiro

Kuwekeza kwa wanawake kuna faida kubwa kwa kizazi hiki na kijacho:Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro, jana amehutibia mkutano wa Umoja wa Afrika unaofanyika mjini Kampala Uganda na kusisitiza vita dhidi ya ugaidi na kuwekeza kwa wanawake.

Bi Migiro amesema zikiwa zimesalia siku 60 kabla ya mkutano wa kimataifa wa malengo ya maendeleo ya milenia mjini New York, Umoja wa Mataifa umejidhatiti kuhakikisha ajenda ya amani na maendeleo Afrika inapewa kipaumbele. Pia ametoa pole kwa serikali na familia za waliouawa katika shambulio la kigaidi wakati wakiangalia kwa njia ya televisheni faianali ya kombe la dunia mjini Kampakla.

Ametoa wito wa juhudi zaidi kufanyika kutekeleza mipango ya Umoja wa mataifa ya kukabiliana na ugaidi, kwa hatua za kimataifa, kutekeleza utawala wa sheria na kuheshimu haki za binadamu. Pia amegusia masuala ya utekelezaji wa malengo ya milenia hasa afya ya mama na motto na kusema kuwekeza kwa wanawake kuna faida kubwa, kwa kizazi hiki na kizazi kijacho.