Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama inayoungwa mkono na UM imemkuta na hatia ya uhalifu wa vita mkuu wa magereza wa Khmer Rouge

Mahakama inayoungwa mkono na UM imemkuta na hatia ya uhalifu wa vita mkuu wa magereza wa Khmer Rouge

Mkuu wa magereza wa zamani wa Khmer Rouge nchini Cambodia Duch amekutwa na hatia ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, na mahakama ya Cambodia ya uhalifu inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Duch mwenye miaka 67 ambaye jina lake kamili ni Kaing Guek Eav amehukumumiwa kwenda jela miaka 35. Alikiri kuhusika na utesaji na mauaji ya maelfu ya wanaume, wanawake na watoto katika gereza la Toul Sleng na ameomba msamaha. Hii ni hukumu ya kwanza kutolewa na mahakama hiyo ya uhalifu.

Waendesha mashitaka waliwataka majaji kutoa kifungo cha miaka 40, hata hivyo Duch hatotumikia kifungo cha miaka 35, kwani majaji walipunguza kifungo chake kwa miaka mitano baada ya kuwa alishikiliwa kinyume cha sheria , na kupunguza tena kwa miaka 11 ambayo tayari amekaa jela. Hivyo Dhuch atatumikia kifungo cha miaka 19 pekee.

Umati wa watu ulifurika nje ya mahakama hiyo mjini Phnom Penh kusikiliza hukumu na baada ya kusomwa wengine walisikika wakisema hakuna haki kwani walitaka Duch aende jela maisha. Lars Olsen ni afisa mawasiliano wa masuala ya kisheria na alikuwa na haya ya kusema baada ya hukumu hiyo.

(SAUTI YA LARS OLSEN)