Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Adha kwa wakimbizi wa Somalia zaonekana kutofikia tamati:UNHCR

Adha kwa wakimbizi wa Somalia zaonekana kutofikia tamati:UNHCR

Wakimbizi wa Kisomali wanakabiliwa na adha kubwa ndani na nje ya nchi yao wanakopata hifadhi.

Hayo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Ukiacha shida ya usalama ndani ya nchi yao, wanabakwa, kukamatwa, kuteswa, kufungwa na hata kurejeshwa kwa nguvu nyumbani kunakowaka moto wa vita.

UNHCR inasema na mashambulio ya karibuni ya kigaidi Afrika mashariki yamezidhisha dhiki kwa wakimbizi hao. Mwandishi wetu Jason Nyakundi amewatembelea baadhi ya wakimbizi hao wanaishi nchini Kenya.