Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wa Gaza wavunja rekodi ya dunia kwenye michezo ya kiangazi ya UNRWA

Watoto wa Gaza wavunja rekodi ya dunia kwenye michezo ya kiangazi ya UNRWA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia wakimbizi wa Palestina UNRWA limesema watoto wa Ukanda wa Gaza wamevunja rekodi ya dunia ya kudunda mpira wa kikapu.

Zaidi ya watoto 7000 wanaoshiriki michezo ya kiangazi inayosimamiwa na UNRWA walishiriki katika juhudi za kuvunja rekodi hiyo. Watoto hao wenye umri wa kati ya miaka 6 na 15, walisimama kwa mpangilio maalumu wa mfumo wa mraba uliotia nakshi kiwanja na kudundadunda mpira wa kikapu kwa dakika 15 bila kupumzika. Mkuu wa operesheni za UNRWA John Ging amewaambia watoto hao tukio hilo ni ujumbe kwa kila mtu kwamba nyie ni watoto shupavu , wenye akili na ni mabingwa wa dunia.

(SAUTI YA JOHN GING)

Mapema wiki hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliwaunga mkono watoto hao kwa njia ya video na kuwapongeza kwa kushiriki michezo ya kiangazi ya UNRWA Gaza na kuwambia kwamba kushiriki kwenu ni kuionyesha dunia kwamba mkipewa nafasi mnaweza kushika namba moja. Rekodi ya awali ya kudunda mpira wa kikapu iliwekwa na jimbo la Indiana nchini Marekani mwaka 2007.