Skip to main content

Nchi za Afrika ya Mashariki zaonekana kuwa kinara wa ufisadi:TI

Nchi za Afrika ya Mashariki zaonekana kuwa kinara wa ufisadi:TI

Umoja wa Mataifa, mashirika ya misaada na wahisani mbalimbali wamekuwa msitari wa mbele kupiga vita ufisadi.

Wadau wote hao wanaungana kusema kuwa rushwa ni adui wa haki na maendeleo katika jamii yoyote duniani. Lakini pamoja na debe lote linalopigwa kwenye nchi za Afrika ya Mashariki inaonekana ufisadi umemea mizizi na hauna dalili ya kuisha leo wala kesho.

Sasa shirika la kimataifa Transparency International (TI) limetoa ripoti inayoziweka mstari wa mbele kwa ufisadi nchi za Afrika ya Mashariki. Nchi hizo ni pamoja na Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda na Tanzania. Je nani kashika nafasi ya ngapi kwa ufisadi? mwandishi wetu Jason Nyakundi anaarifu kutoka Nairobi.