Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wananchi wa Burundi wahitimisha uchaguzi kwa kura ya wabunge leo

Wananchi wa Burundi wahitimisha uchaguzi kwa kura ya wabunge leo

Huko Burundi wananchi wamehitimisha mchakato wa uchaguzi mkuu kwa kupiga kura ya kuchagua wabunge leo.

Watu milioni tatu unusu wameshiriki katika uchaguzi leo wa wabunge ikiwa ni hatua za mwishomwisho za mchakato wa chaguzi mbalimbali. Wagombea kutoka vyama saba wanawania Viti 100 bungeni.Hata hivo chama tawala kinaelekea kupata ushindi mkubwa baada ya wapinzani kususia mchakato mzima wa uchaguzi.

Uchaguzi huo unafuata ule wa Rais uliofanyika tarehe 28 ya mwezi uliopita baada ya kutanguliwa na uchaguzi wa udiwani uliozua utata na hata vyama vingi ya upinzani kujitoa kwenye mchakato mzima wa uchaguzi mkuu. Kutoka Bujumbura,muaandshi wetu Ramadhani Kibuga ametutumia taarifa hii.