Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu la UM kuchunguza shambulio la flotilla Gaza

Baraza la haki za binadamu la UM kuchunguza shambulio la flotilla Gaza

Rais wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa balozi Sihasak Phuangketkeow amewateuwa wataalamu watatu kushiriki tume binafsi ya kimataifa ili kuchunguza shambulio la flotilla Gaza.

Tume hiyo itatafuta ukweli kuhusu ukiukaji wa sheria za kimataifa ikiwemo masuala ya kibinadamu na haki za kimataifa za binadamu. Wataalamu hao ni pamoja na jaji Karl T. Hudson-Phillips, Sir Desmond de Silva na Mary Shanthi Dairiam.

Akitangaza kuteuliwa kwao balozi Sihasak amesema utalaamu, uhuru na kutotegemea upande wowote kwa wataalamu hao kutasaidia kupata ukweli wa tukio la mwezi Machi na uhalali wake kisheria. Na ametoa wito kwa pande zote husika kutoa ushirikiano kwa tume hiyo akitumaini kwamba mpango huo utachangia kuleta amani kwenye eneo hilo na haki kwa waathirika wa shambulio la flotilla.