Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya usalama Kaskazini mwa Yemen bado ni tete yasema UNHCR

Hali ya usalama Kaskazini mwa Yemen bado ni tete yasema UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema zaidi ya miezi mitano kukiwa na makubaliano ya kusitisha vita na ikiwa ni mwezi mmoja tangu makubaliano mapya ya amani ya alama 22 kutiwa saini, hali ya usalama bado ni tete Kaskazini mwa Yemeni.

UNHCR inasema wanakadiria kwamba hadi sasa wakimbizi wa ndani zaidi ya elfu kumi ndio waliorejea huku kukiwa na wakimbizi wa ndani zaidi ya laki tatu.

Ukosefu wa huduma muhimu kama za afya, elimu na maji safi katika jimbo la Sa'ada vimeelezwa kuwavunja watu moyo wa kurejea katika maeneo hayo. Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA MELISA FLEMING)