Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Je tusubiri hadi vifo zaidi vitokee kutokana na baa la njaa Sahel:UM

Je tusubiri hadi vifo zaidi vitokee kutokana na baa la njaa Sahel:UM

Matatizo makubwa ya chakula katika eneo la Sahel hivi sasa yanatishia maisha ya watu milioni 10 wakiwemo maelfu ya watoto.

Wafanyakazi wa misaada wanahitaji msaada wa kimataifa ili kukabiliana na hali hiyo kabla haijawa zahma kubwa. Niger moja ya nchi masikini kabisa duniani na watu milioni 7.1 wameathirika na baa la njaa. Nchi jirani ya Chad watu milioni 2 wanahitaji msaada wa chakula, huku maelfu wengine katika nchi za Mali, Burkina Faso na sehemu ya Kaskazini mwa Nigeria wanahangaika kuweza kuishi.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya FAO, UNICEF, OCHA na WFP na shirikisho la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu IFRC wote wameonya kuhusu hali hiyo ya hatari.

Mashirika hayo yamezitaka serikali, sekta binafsi, na raia wa kawaida kuchangia, kwani kila senti ni muhimu, ili kuepusha janga kubwa litakalogharimu maisha ya watu wengi.