Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imetoa tahadhari kuhusu wanavyotendewa wakimbizi wa Kisomali

UNHCR imetoa tahadhari kuhusu wanavyotendewa wakimbizi wa Kisomali

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetahadharisha kuhusu kuendelea kuzorota kwa jinsi wanavyotendewa wakimbizi wa Kisomali ndani ya Somalia na maeneo jirani.

Shirika hilo linasema ongezeko la mashambulizi ya kibaguzi yanawatia hofu ya mazingira ya kuwalinda wakimbizi hao katika pembe ya Afrika na katika bara zima. Wakimbizi hao wamekuwa wakiarifu kusumbuliwa kwa maneno na vitendo, kukamatwa, kutiwa mahabusu, kurejeshwa kwa nguvu na hata kuteswa.

UNHCR inasema hofu yao kubwa ni hatua ya uongozi wa Puntland wa kuwarejesha katikati mwa Somalia kwa nguvu. Zaidi ya wakimbizi wa ndani 900 Jumanne na Jumatano wiki hii.

Katika mji wa Gaalkacyo ambako baadhi ya wakimbizi waliorejeshwa wanahifadhiwa, wengi wakiwa wanaume wa umri wa kati ya miaka 18 na 25, UNHCR inawasaidia kwa chakula, maji, madawa na mablanketi. Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR anafafanua kuhusu hofu yao.

(SAUTI YA MELISA FLEMING)