Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu asema, utatuzi wa mgogoro wa Israeli na Palestina utanufaisha wananchi wake

Katibu Mkuu asema, utatuzi wa mgogoro wa Israeli na Palestina utanufaisha wananchi wake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki Moon amesema utatuzi wa mgogoro wa nchi mbili za Israeli-Palestina zitanufaisha Waisraeli na Wapalestina.

Ban amesema hayo kupitia ujumbe wake alioutuma kwenye warsha ya kimataifa ya amani ya Mashariki ya Kati inayoendelea mjini Lisboni nchini Ureno, ambayo inaangalia nafasi ya Wanawake wa Israeli na Palestina katika kuleta amani na usalama ndani ya Mashariki ya kati. Amesema utatuzi wa mgogoro huo utakuwa na maslahi pia kwa jumuiya ya kimataifa.