Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tamko la Kosovo kuwa huru halikukiuka matumizi ya sheria za kimataifa: UM

Tamko la Kosovo kuwa huru halikukiuka matumizi ya sheria za kimataifa: UM

Umoja wa Mataifa umetoa tamko la ushauri juu ya suala la Mahakama ya kimataifa kubainisha kuwa tamko la Kosovo la upande mmoja lililotolewa na Serbia mwaka 2008, halikukiuka sheria za kimataifa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki Moon, kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake amezitaka pande zote kujihusisha na mazungumzo yatakayo leta muafaka na kuepuka masuala yoyote yanayoweza kuleta mfarakano katika mazungumzo hayo.

Vilevile Ban amesema atapeleka shauri lake katika Baraza Kuu ambalo litashughulikia namna ya kuendelea na suala hilo.

Kwa kura kumi dhidi ya nne, majaji wa mahakama ya kimataifa walihitimisha kwamba tamko hilo halikiuki sheria za kimataifa, azimio la Baraza la Usalama la mwaka 1999 kufuatika kumalizika mapigano ya Kosovo, wala rasimu ya katiba. Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa Jaji Hisashi Owada amesema

(SAUTI YA JAJI OWADA)