Skip to main content

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anakutana na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anakutana na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron. Hii ni ziara ya kwanza ya Waziri Mkuu huyo mpya wa Uingereza kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Katika mazungumzo yao wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo suala la Afghanistan, hali ya mashariki ya kati, mabadiliko ya hali ya hewa na maandalizi ya mkutano wa kimataifa wa malengo ya maendeleo ya millennia utakaofanyika mwezi Septemba kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York.

Katibu Mkuu amepongeza kiwango cha hali ya juu cha serikali ya Uingereza katika kuhakikisha inatimiza malengo ya milenia na amesema anatumaini kwamba hatua hiyo ya Uingereza na msimamo wake unaweza kuwa mfano kwa nchi nyingine kufuata nyayo.