Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya Kimataifa imetoa hukumu leo kuhusu hatma ya kesi ya Kosovo

Mahakama ya Kimataifa imetoa hukumu leo kuhusu hatma ya kesi ya Kosovo

Mahakama ya kimataifa ya haki leo imetoa ushauri wa maoni kuhusu uhalali wa azimio la mwaka 2008 la Kosovo kujitangazia uhuru wake kutoka Serbia na kuamua kwamba kujitanda na kua huru kwa Kosovo si kukiuka sheria.

Wajumbe 69 wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Marekani na nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Ulaya hivi sasa wanautambua uhuru wa Kosovo. Wale wanaoupinga ni pamoja na Serbia, Urusi, Uchina, India na Hispania.

Uamuzi wa kuunga mkono uhuru wa Kosovo utasaidia kwa mataifa mengine zaidi kutambua nchi hiyo. Lakini Serbia inataka Kosovo irejee kuungana na nchi hiyo na wanaounga mkono uamuzi wa Serbia na kusema kuruhusu kujitenga kwa Kosovo kutachagiza sehemu zingine duniani kutaka kujitenga pia.