Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM wanahofia hatma ya mahabusu walioko Guantanamo

Wataalamu wa UM wanahofia hatma ya mahabusu walioko Guantanamo

Wataalamu wawili wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wanasema Marekani isiwarejeshe kwa nguvu Algeria mahabusu wawili wanaoshikiliwa Guantanamo Bay.

Martin Schenin mwakilishi maalumu kuhusu masuala ya haki za nbinadamu na vita dhidi ya ugaidi, na Manfred Nowak mwakilishi kuhusu masuala ya utesaji wamesema wanahofia kwamba maisha ya mahabusu wawili wa Algeria walioko Guantanamo yanaweza kuwekwa hatarini. Bwana Nowark amelezea sababu ya hofu yao.

(SAUTI YA NOWARK)

Ameongeza kuwa utesaji hufanyika kwa siri na serikali haziwezi kudhibiti vitendo vya maafisa wa usalama na upelelezi.