Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu milioni 10 wanakabiliwa na baa la njaa eneo la Sahel Afrika:UM

Watu milioni 10 wanakabiliwa na baa la njaa eneo la Sahel Afrika:UM

Umoja wa Mataifa unasema matatizo ya njaa yanawaathiri watu zaidi ya milioni 10 katika eneo la Sahel Afrika ambalo limekumbwa na ukame, na watu hao wanahitaji msaada wa haraka.

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa John Holmes amewataka wahisani kuchangoa dola milioni 230 zaidi ili kuwasaidia watu wazima na watoto nchini Niger, Mali, Chad, Mauritania, Burkina Faso, Cameroon Kaskazini na Nigeria Kaskazini.

Ameongeza kuwa chakula kinahitajika haraka ili kuokoa maisha yao na mifugo yao. Amewaambia nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kwamba msaada unahitajika haraka ili kuepusha alichokiita janga kubwa la kibinadamu kama.