Skip to main content

ILO inazindua utekelezaji wa mapendekezo mapya ya HIV na kazi

ILO inazindua utekelezaji wa mapendekezo mapya ya HIV na kazi

Shirika la kazi duniani ILO linafanya mfululizo wa matukio mbalimbali chini ya kauali mbiu "kuzuia HIV kulinda haki za binadamu kazini" kwenye mkutano wa kimataifa wa ukimwi 2010 ili kuzindua mapendekezo mapya.

ILO itajikita katika kuunda ushirika imara na jumuiya ya kimataifa ya wahisani, wadau wanao tekeleza sera za HIV na mipango ya watu wanaoishi na virusi vya HIV.

Lengo ni kupunguza unyanyapaa na ubaguzi kwa wafanyakazi wote wanaoishi na virusi vya HIV au wanaoaminika kuwa na virusi, lakini pia kutoa mtazamo mpya katika juhudi za kuzuia ugonjwa huo na kuhakikisha azimio linatekelezwa na serikali, waajiri na wafanyakazi wenyewe.