Nigeria inavutia wahamiaji lakini inapoteza wataalamu wake: IOM
Taarifa ya uhamiaji ya Nigeria iliyotolewa leo na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM inasema, nchi hiyo bado ni kivutio kikubwa cha wahamiaji wa kikanda ,ingawa idadi kubwa ya wataalamu wake wanaenda kutafuta kazi ng\'ambo.
Kwa mujibu wa tume ya idadi ya watu nchini humo, idadi ya wageni wanaohamia Nigeria imeongezeka zaidi ya mara mbili katika miongo ya karibuni kutoka 477,135 mwaka 1991 na kufikia 971,450 mwaka 2005.
Takwimu hizo zinaonyesha kwamba wahamiaji wengi wanatoka katika nchi jirani za jumuiya ya ushirikiano wan chi za Afrika Magharibi ECOWAS na wengi wanaingia nchini humo kutafuta kazi na maisha bora.