WFP inaandaa mipango kabambe kusaidia baa la njaa nchini Niger

WFP inaandaa mipango kabambe kusaidia baa la njaa nchini Niger

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP leo limesema linaongeza juhudi zake za msaada wa chakula nchini Niger ili kuwalisha watu wapatao milioni nane wanaokabiliwa na njaa.

Njaa imeikumba nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi baada ya msimu wa mvua za masika kutonyesha ipasavyo, na kusababisha watu kupoteza mazao yao na mifugo pia. Mkurugenzi wa WFP Josette Sheeran amesema tatizo la baa la njaa linaongezeka nchini humo na idadi ya wanaohitaji msaada sasa ni kubwa.

Bi Sheeran ambaye ameanza ziara nchini humo leo amesema anataka kujionea mwenyewe mahitaji ya watu wa Nigera na changamoto zinazolikabili shirika lake kwa ajili ya shughuli ya kuokoa maisha ya watu Nigera na hususan watoto.