Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon anaelekea Afghanistan kwa ajili ya mkutano wa kimataifa kesho

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon anaelekea Afghanistan kwa ajili ya mkutano wa kimataifa kesho

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anaelekea Afghanistan ambako kesho pamoja na Rais Hamid Karzai atakuwa mwenyekiti mwenza katika mkutano wa kimataifa kuhusu nchi hiyo.

Ban atatoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo ambapo anatarajiwa kutoa wito kwa watu wa Afghanistan kuungana pamoja ili kupata amani kwa njia ya maridhiano na kujenga mustakhbali wa taifa lao kwa kuzingatia maendeleo ya kiuchumi na ushirikiano kwa kuheshimu uhuru wa taifa lao.

Ban pia anatarajiwa kuwaomba Waafghanistan kuungan kwa maslahi ya taifa lao. Akiwa mjini Kabul kesho Katibu Mkuu atakutana na Rais Karzai na maafisa wengine wa serikalui watakaokuwa wakihudhuria mkutano. Na baadaye yeye na Rais Karzai watazungumza na waandishi wa habari.