Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Ulaya umechangia euro milioni 2 kwa michezo ya UNRWA

Umoja wa Ulaya umechangia euro milioni 2 kwa michezo ya UNRWA

Umoja wa Ulaya leo umetangaza kuchangia Euro milioni mbili kusaidia michezo ya kiangazi kwa watoto wa Gaza inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia wakimbizi wa Palestina UNRWA.

Fedha hizo pia zitatumia kusaidia mipango ya UNRWA ambayo ni muhimu kwa kuboresha huduma za shirika hilo. Euro milioni moja kati ya hela hizo zitasaidia makambi 12000 ya kmichezo ya kiangazi kwa kipindi cha wiki nane, yakiwa na watoto 250,000. Wakati huohuo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametuma ujumbe kwa njia ya video kwa watoto wa Gaza akiwapongeza kwa kushiriki michezo hiyo ya kiangazi.

Amesema kwa kushiriki kwao wanaoinyesha dunia kwamba wakipewa fursa wanaweza kushika namba moja. Ban pia amewashukuru wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa Gaza kwa kuandaa michezo hiyo na kwa kuwasaidia watoto wa Gaza kuonyesha kwamba wanaweza kuruka viunzi vya aina yoyote ile na kuwa bora duniani.