Skip to main content

UM unatarajia hatua za maridhiano zaidi kutoka serikali ya Cuba:Ban

UM unatarajia hatua za maridhiano zaidi kutoka serikali ya Cuba:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kuwepo kwa hatua zaidi za maridhiano kutoka kwa serikali ya Cuba.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari leo mjini Geneva Ban amesema Umoja wa Mataifa bado unatarajia serikali ya Cuba kuchukua hatua zaidi za maridhiano, kuanzisha utawala wa sheria na kuheshimu haki za binadamu.

Ban pia amezungumzia sula la mvutano baina ya Venezuele na Colombia ambapo amesisitiza kuwa mvutano huo utatuliwe kwa njia ya amani na mazungumzo. Na akaongeza endapo kuna ombi lolote litatolewa na pande hizo basi Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa msaada wa kiufundi.