Skip to main content

Nelson Mandela shujaa wa Afrika na dunia aenziwa kimataifa Julai 18

Nelson Mandela shujaa wa Afrika na dunia aenziwa kimataifa Julai 18

Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza unaungana na dunia nzima Julai 18 kumuenzi na kutamini mchango wa Nelson Mandela aliyekuwa Rais wa kwanza Mwafrika nchini Afrika ya Kusini.

Mandela anaenziwa kwa mchango wake mkubwa wa kutokomeza ubaguzi wa rangi, kupigania haki na kutafuta demokrasia.

Na makala yetu maalumu leo inaungana na dunia nzima kumuenzi shujaa huyu wa ukombozi kwa  kuzungumza na Dr Salim Ahmed Salim aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa afrika kwa muda mrefu akichambua na Flora Nducha umuhimu wake na siku hii maalumu.