Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani mashambulio ya kujitoa muhanga nchini Iran

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani mashambulio ya kujitoa muhanga nchini Iran

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulio mawili ya kujitolea muhanga karibu na msikiti mjini Zahedan mji mkuu wa jimbo la Sistan-Baluchistan kusni mashariki mwa Iran.

Zaidi ya watu 20 wamearifiwa kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa kwenye mashambulio hayo yaliyotokea jana. Katika taarifa yake leo kupitia msemaji wake, Ban amesema vitendo hivyo vya kigaidi visivyo na maana kwenye maeneo ya kuabudu vinachefua zaidi.

Ban ametoa salamu za rambirambi kwa familia za waliouawa na waliojeruhiwa amewatakia nafuu ya haraka, pia ametoa pole kwa serikali na watu wote wa Iran.