Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO leo imetoa taarifa ya hali ya afya ya Jamhuri ya watu wa Korea DPRK

WHO leo imetoa taarifa ya hali ya afya ya Jamhuri ya watu wa Korea DPRK

Shirika la afya duniani WHO leo limetoa takwimu za afya za Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea.

Takwimu hizo zinaonyesha kwamba matatizo makubwa ni pamoja na idadi kubwa ya vifo vya kina mama na watoto, utoaji mimba, utapia mlo kwa watoto, na idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa na uzito mdogo jambo linaloashiria lishe duni.

Pia WHO imebaini kuwa usambazaji wa dawa za uzazi wa mpango ni mdogo, jambo linalochangia kiasi kikubwa cha utoaji mimba. Pia matatizo ya kupata dawa na vifaa yamefanya magonjwa kama kifua kikuu, malaria na hepatitis B kuwa ni matatizo ya kudumu. Paul Garwood ni afisa wa WHO

(SAUTI YA PAUL GARWOOD)