Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Changamoto za Guinea-Bisau lazima zitatuliwe bila kuchelewa:UM

Changamoto za Guinea-Bisau lazima zitatuliwe bila kuchelewa:UM

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa amesema matukio ya karibuni nchini Guinea-Bissau yametia dosari juhudi za kujeresha utulivu katika nchi hiyo, lakini changamoto hizo zinaweza kukabiliwa endapo zitashughulikiwa haraka bila kuchelewa.

ApriIi mosi mwaka huu vikosi vya jeshi ambavyo vilikuwa chini ya uongozi wa naibu mkuu wa majeshi jenerali Antonio N' djai vilichukua udhibiti wa makao makuu ya jeshi, kumshikilia mkuu wa majeshi, makamu wa amiri jeshi mkuu Zamora Induta na kwa muda mfupi walimshikilia waziri mkuu Carlos Gomez Junior. Pia siku hiyo wanajeshi waliokuwa na silaha waliingia kwa nguvu kwenye majengo ya Umoja wa Mataifa mjini Bissau wakidai kuachiliwa mara moja kwa msaidizi wa mkuu wa majeshi Bubo Na Tchto ambaye aliondoka kwenye majengo hayo baada ya kutia sahihi taarifa kwamba anaacha jeshi kwa hiyari na kwa amani.

Akiwasilisha taarifa kwenye baraza la usalama mwakilishi maalumu wa Ban Ki-moon nchini humo Joseph Mutaboba amesema matukio hayo ya Aprili mosi ambayo yalikiuka katiba, pia kuikosea jumuiya ya kimataifa kwa kuingilia ofisi za Umoja wa Mataifa, yameingilia pakubwa juhudi za mchakato wa amani nchini humo.