Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa unasherehekea Siku ya Nelson Mandela kumuenzi raia huyo ambaye ni mfano wa kimataifa

Umoja wa Mataifa unasherehekea Siku ya Nelson Mandela kumuenzi raia huyo ambaye ni mfano wa kimataifa

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo limefanya kikao kisicho rasmi kuienzi kwa mara ya kwanza siku ya kimataifa ya Nelson Mandela ambayo itakuwa Jumapili Julai 18.

(MUSIC)

Nelson Mandela ambaye anasherehekea mika 92 ya kuzaliwa Jumapili hii, ni shujaa wa kupinga ubaguzi wa rangi, na siku yake inaadhimishwa wiki moja tuu baada ya kufanyika mashindano ya kombe la dunia nchini Afrika ya Kusini yaliyokuwa mafanikio makubwa.

Kwa mara ya kwanza dunia mwaka huu itaungana naye kusherehekea siku hiyo ya kimataifa iliyoafikiwa na uamuzi wa Umoja wa Mataifa Novemba mwaka jana. Mwaka 1994 alipozungumza kwenye Umoja wa Mataifa baada ya kutoka jela Madela aliushuruku Umoja huo kwa juhudi zake.

(SAUTI YA MANDELA)

Siku hii ambao ni siku yake ya kuzaliwa Julai 18 kuanzia sasa itakuwa ni siku ya kimataifa kuenzi na kuthamini mchango wake katika kutafuta amani na uhuru jambo amablo Mandelela amekiri lilichukua muda kufikiwa

(SAUTI YA MANDELA 2)

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa kutambua, kuheshimu na kuthamini mchango wa Mandela mtu huyu ambaye ni wa kawaida kabisa, amefanya mambo makubwa yatakayokumbukwa daima, amesema Ban.

(SAUTI YA BAN)

Nao mpango wa Umoja wa Mataifa Darfur katika kuenzi siku hiyo watakuwa na mechi ya kandanda kwa ajili ya amani.