Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kitengo cha msaada wa maendeleo vijijini cha Umoja wa Mataifa kinasaidia kukabiliana na njaa Niger

Kitengo cha msaada wa maendeleo vijijini cha Umoja wa Mataifa kinasaidia kukabiliana na njaa Niger

Kitengo cha Umoja wa Mataifa cha maendeleo vijijini kinasaidia kuimarisha mipango ya kilimo katika jimbo la Sahel Afrika ya Magharibi na hususan Niger ambayo sasa inamatatizo makubwa ya chakula.

Kujirudia kwa matatizo ya chakula kumeliathiri eneo la Sahel ikiwa ni pamoja na nchi za Burkina Faso, Chad, Eritrea, Mali, Mauritania, Niger, Senegal na Sudan. Ukame mbaya katika eneo hilo ulikuwa mwaka 2005 ambapo watu milioni moja walikufa na wengine milioni 50 kuathirika.

Kutokana na kutonyesha ipasavyo kwa mvua za masika watu milioni 7.6 nchini Niger ambao ni karibu nusu ya watu wote wanakabilia na upungufu mkubwa wa chakula.

Kwa mujibu wa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD familia nyingi katika jimbo la Maradi zinategemea msaada ili kujikimu.