UM unakabiliwa na upungufu wa dola bilioni 5 kwa shughuli zake za kibinadamu

UM unakabiliwa na upungufu wa dola bilioni 5 kwa shughuli zake za kibinadamu

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wake wanakabiliwa na upungufu wa dola bilioni tano mwaka huu za kuweza kukabiliana na matatizo ya kibinadamu yanayoikumba dunia.

Hata hivyo mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya misaada ya kibinadamu John Holmes amesema pamoja na msukosuko wa kiuchumi ulioikumba dunia mwaka huu kuweza kuendelea na kusaidia bajeti ya misada ya kibinadamu mwaka huu ni mafanikio makubwa kwa wahisani wengi.