Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makubaliano ya kufuta madeni kusaidika kukabili kifua kikuu Indonesia

Makubaliano ya kufuta madeni kusaidika kukabili kifua kikuu Indonesia

Australia, Indonesia na mfuko wa kimataifa Global Fund wamesaini makubaliano muhimu ambayo yataongeza msaada wa mipango ya kupambana na kifua kikuu nchini Indonesia.

Indonia inashika nafasi ya tatu kwa kuwa na waathirika wengi wa kifua kikuu duniani, na raia wake 90,000 hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huo. Licha ya kwamba ugonjwa huo unaweza kukingwa na kutibika, nchini Indonesia idadi ya wagonjwa inaongezeka kama katika nchi nyingine zinazoendelea.

Katika maafikiano hayo chini ya mpango wa madeni kwa afya (Debt2health) Australia itaifutia Indonesia deni la dola milioni 75 za Australia, kwa masharti kwamba Indonesia itawekeza nusu ya fedha hizo katika mipango ya taifa ya kukabiliana na kifua kikuu kwa kupitia mfuko wa kimataifa unaopambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria.