Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa kilimo nchini Haiti unahitaji msaada zaidi kuimarika:FAO

Mfumo wa kilimo nchini Haiti unahitaji msaada zaidi kuimarika:FAO

Mratibu wa masuala ya dharura na usaidizi wa shirika la kilimo na chakuala FAO nchini Haiti Etienne Peterschmitt amesema wakati msaada wa chakula na bidhaa za kilimo viliisaidia sana nchi hiyo baada ya tetemeko, msaada zaidi unahitajika katika sekta ya kilimo.

Amesema upungufu wa fedha za kusaidia sekta ya kilimo nchini humo unaendele kurudisha nyuma juhudi za kukabiliana na tatizo la chakula, uzalishaji na fursa za kiuchumi katika maeneo ya vijijini ikiwa ni miezi sita sasa baada ya tetemeko hilo.

Peterschimitt amesema uwekezaji katika kilimo, na fursa za ajira vijijini vinahitajika kwa haraka ili kuzuia idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani kurejea tena Port-au-Prince na pia kusaidia usalama wa chakula nchi nzima. Amesema misaada mingi imekuwa ikilenga zaidi maeneo ya mijini, lakini jumuiya ya kimataifa isiyasahau maeneo ya vijijini kama kweli wanataka kukabiliana na athari zilizosababishwa na tetemeko nchini Haiti.